Sunday, November 25, 2012

MARAIS WA AFRIKA MASHARIKI WAIJADILI DRC


Mkimbizi wa Goma akiingia kambi ya Umoja wa Mataifa nje ya Goma
Wapiganaji mashariki mwa Congo walisonga mbele zaidi ndani ya ardhi iliyokuwa ikidhibitiwa na jeshi la serikali siku ya Alkhamisi.


Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa awali juma hili iliishutumu Rwanda kuwa inawasaidia wapiganaji hao, shutuma ambazo zinakanushwa na serikali ya Rwanda.
Kiongozi wa kiraia wa kundi la wapiganaji wa M23 piya yuko kwenye mkutano wa Kampala.
Haijulikani mchango wake ni wa kiasi gani kwenye mkutano huo wa dharura wa viongozi wa kanda ya Maziwa Makuu.
Wapiganaji wanataka kuzungumza ana kwa ana na serikali ya Congo.
Lakini Rais Joseph Kabila anasema atazungumza tu na Rwanda.
Huku nyuma wapiganaji wanaendelea kusonga mbele wakielekea kusini na kaskazini kutoka shina lao mjini Goma.
Umoja wa Mataifa unasema kikosi chake kilioko huko kitajaribu kuwazuwia wapiganaji wasisonge mbele, lakini umesema askari wake wa kuweka amani hawawezi kubeba jukumu la jeshi la serikali ya Congo.

No comments:

Post a Comment