Mkutano Mkuu wa chama kinachotawala nchini Tanzania CCM unamalizika leo
huko Dodoma, ambapo miongoni mwa mambo yaliyojitokeza katika siku ya
mwisho hii leo ni suala la amani na katiba mpya hususan visiwani
Zanzibar
Rais wa zamani wa Zanzibar ambaye amemaliza muda wake kama makamu
mwenyekiti wa chama tawala nchini CCM hapo jana (13.11.2012) Amani Abeid
Karume amejivunia mafanikio aliyosimamia visiwani humo wakati wa
utawala wake.
Pamoja na kwamba baadhi ya mila za Kiafrika zinataka mwanaume awe na
watoto wengi na wa kiume kama mrithi, wanaume wa Afrika wameanza
kubadilika kwa kuachana na mila hizo baada ya kutambuwa umuhimu wa uzazi
wa majira.